In Kiswahili

Ni zaidi ya jitihada za mabadiliko na umoja wa ulimwengu mzima kutoka kwa wadau wote na hasa wale wa sekta ya ujenzi zinahitajika kwa jamii ya binadamu ili kufanikiwa katika maendeleo endelevu, na katika kupunguza athari mbaya za mabadiliko ya hali ya hewa katika ngazi za kimataifa na kitaifa.

Ukuaji wa idadi ya watu duniani na ukuaji kasi wa miji unahitaji shughuli kubwa za ujenzi na matumizi makubwa ya vifaa vya ujenzi. Ndani ya miaka kumi ijayo, mahitaji ya jumla ya matumizi ya ardhi ya mazingira yaliyojengwa duniani yanatarajiwa kuongezeka mara dufu. Istoshe, inatarajiwa kwamba katika nchi zenye uchumi ulioendelea zaidi, miundombinu na utunzaji wa majenzi utaongezeka sana. Vitendo vya sasa vya usimamizi wa ujenzi na majenzi havijafikia kuwa endelevu. Ikiwa haya hayatabadilishwa, uzalishaji wa hewa chafu kutoka sekta ya ujenzi pekee utahatarisha kufanikiwa kwa malengo ya makubaliano ya Paris.

Kuelekeza upya sekta ya ujenzi kuna changamoto kubwa ambayo inahitaji mlengo wa kisiasa wenye nguvu na stahimilivu. Sekta ya ujenzi imepangiliwa kwa mtawanyo wa madaraka ikijumuisha idadi kubwa ya mashirika na washiriki. Kuna mifumo kidogo au hakuna kabisa mfumo jumuishi kati ya watoa huduma au wamiliki na wateja. Aidha, ukuzaji wa teknolojia inayotumika unaongezeka, na viwango, kanuni, na miongozo ya kimataifa inayotawala usanifu na ujenzi wa mazingira yaliyojengwa hubadilika polepole mno kuendana na maendeleo ya kiteknolojia yanayoongezeka kwa kasi.

GLOBE inavuta umakini wa wafanya maamuzi wa jamii juu ya uhitaji wa njia mpya bora zitakazotekelezwa na wadau wote na kupitia viungo vyote vya minyororo ya thamani ya sekta ya ujenzi. Wawezeshaji wakuu wa mabadiliko haya ya kimageuzi wanabainiwa kama maboresho lengwa ya kanuni na sheria, motisha za kifedha pamoja na utafiti na elimu. Vyombo vya uendeshaji vilivyopendekezwa kwa usimamizi wa usanifu na uadilifu wa majengo na miundombinu ni pamoja na kuzingatia dhahiri uchumi mviringo, tathmini ya athari za mazingira kwa mzunguko wa maisha, ongezeko la utumiaji wa modeli na njia za uchambuzi za hali ya juu, vilevile matumizi lengwa ya teknolojia mpya ya utambuzi, uchakataji data na utunzaji.

Ili kuunga mkono uamuzi wa utungaji sera katika ngazi za kimataifa na kitaifa, Kamati ya Pamoja ya Usalama wa Majenzi inatoa msaada wake na inapendekeza kuanzisha Kikosi Kazi cha Wataalam wa Kimataifa chini ya udhamini wa Kamati ya Uhusiano inayojumuisha wataalam kutoka RILEM, IABSE, fib, CIB, ECCS, IASS, na wakisaidiana na mashirika mengine muhimu na yaliyojitolea, ya kimataifa na kitaifa ambayo pia yanaunga mkono GLOBE.

Wanachama wa GLOBE wanafahamu hasa kuwa mazingira yaliyojengwa ni zaidi ya majenzi na miundombinu – inajumuisha na inahusisha jamii kwa ujumla, mazingira, na anuwai pana ya viwanda na taaluma. Ni lengo kuwa mpango wa GLOBE utabadilika kadri muda unavyokwenda ili kuwawajibikia zaidi wadau wote wa mazingira yaliyojengwa, na michango yako katika kuunga mkono hili inakaribishwa kwa dhati na kwa matarajio.

Bofya hapa kwa maelezo zaidi kuhusu GLOBE